tangazo

Thursday, 22 May 2014

WAZIRI WA MALAWI AJIUWA KWA KUSHINDWA KATIKA UCHAGUZI

   Waziri mmoja nchini malawi amejiua  baada ya kupoteza kiti chake cha ubunge polisi wa nchi hiyo wamesema. Naibu huyo wa serikali za mitaa  Godfrey kamanya alijiua kwa kujipiga risasi nyumbani kwake lilongwe  na kuacha ujumbe kwa rais Joyce Banda kuwa amlee na kumsomesha.

                  wasimamizi wa uchaguzi wakiwa kazini kaika vituo vya kupia kura

  Msemaji wa mbunge huyo alikanusha kama huyo Godfrey kamanya alijiua baada ya kukikosa kiti cha ubunge alichokuwa akikitetea. Hata hivyo matokeo ya uchaguzi huo bado hayajatangazwa lakini uchaguzi huo huo ulikuwa ni wenye ushindani sana.

No comments: