tangazo

Wednesday, 6 November 2013

DIAMOND AFUNGUKA NA KUWEKA WAZI SABABU YA KUTOTUMIA KINGA


          Diamond platnumz 
Diamond hakauki kwenye ulimwengu wa habari,staa huyo bongo fleva ameibua mapya na kusema hapendi kabisa kutumia kinga awapo faragha akiwa na warembo wake.diamond katika maelezo yake alionesha wazi suala la afya kwake sio ishu sana ila kilio chake ni mtoto.
      KILIO  CHA MTOTO
 Diamond anasistiza kuwa kiu yake kubwa kwa sasa ni mtoto na si vinginevyo."Nashukuru maisha yanakwenda vizuri lakini nitakuwa mwenye furaha zaidi kama nitabahatika kupata mtoto mwanamke atakaenizalia atakuwa amekamilisha furaha yangu.hitmaker huyo wa my number one amesema siku atakayokuwa akiitwa baba atakuwa amefungua ukurasa mpya kabisa wa maisha yake.
   Ni furaha yangu kuitwa baba unajua huwa naangalia kuna baadhi ya marafki zangu tayari wamepata watoto hata wasafi kuna madensa wangu wama watoto nahisi na mimi nitakuwa na amani nikipata mtoto.
 VIPI KUHUSU MAGONJWA
 Pamoja na kiu yake ya kupata mtoto kutotomia kinga kunamuweka katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa harari ukiwemo ukimwi alisema hana wasi wasi anajiamini na akaongeza kuwa huwa anapima ukimwi mara kwa mara kwa hiyo anajiamini asilimia mia.
  WALIOPITA KWA DIAMOND
Diamond aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na  wasichana kadhaa kati yao  wapo walokubali lakini kuna wengine walikana ikabaki kuwa siri yao.
Baadhi ya wasichana waliowahi kuwa penzini na diamond  ni pamoja na 
         Jacqline wolper

        Wema sepetu



        Joketi mwongelo


        Rehema Fabian 

      Pendo mushi

         Penny
Hawa ni baadhi ya wasichana ambao washawahi lipotiwa kuwa na mahusiano na diamond baadhi yao walishawahi kukiri kubebe mimba ya diamond lakini mwisho wa siku ikawa kimya na ikasemekana mimba zao zimeharibika.

No comments: