tangazo

Wednesday, 18 December 2013

MASHABIKI WAOMBA COLLECTION YA MANGWAIR

        Marehemu Albert mangwair 

 Mashabiki wa msanii nyota aliyefariki mapema mwaka huu Albert mangwair wamemtaka mtayarishaji wa muziki p funky kutengeneza collection ya nyimbo za mkali huyo wa freestyle kama njia ya kumkumbuka na kuisaidia familia yake kimapato.
 Wakizungumza na blog hii kwa nyakati tofauti baadhi ya mashabiki wa msanii huyo walisema kazi za msanii huyo bado zinafanya vizuri hivyo kama zikikusanywa na kutengeneza collection zinaweza kuuza na hivyo kuisaidia familia ya mangwair.hata hivyo jitihada za kumtafuta prodyuza P funky ili aelezee kama wana mpango wa kufanya hazikuweza kufanikiwa

       Prodyuza p funky aliechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya msanii Albert mangwair .

No comments: