Kwa mujibu wa ripoti kutoka mtandao wa TMZ msanii huyo alijikuta akitimuliwa kwenye hoteli baada ya mashabiki wake kuleta fujo na kufanya uharibifu kwa kupiga mawe hotelini wakitaka kumwona msanii huyo.
Baada ya tukio hilo msanii huyo kupitia mtandao wa kijamii wa twitter akiwaomba mashabiki wake waliopo kwenye ile hoteli watulie,
"Kwa mashabiki wangu mliopo hotelini ahsanteni sana na nawapenda sana lakini tafadhali naomba mtulie na muwaheshimu polisi hatutaki mtu yeyote aumie"
Mashabiki wa beiber walijikuta wakipiga kambi nje ya hoteli ya faena ambayo msanii alifikia na uongozi wa hoteli hiyo ulishindwa kuvumilia baada ya mashabiki hao kuanza kuharibu vitu na mali katika hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment