NAPE AMWITA MBATIA MNAFIKI KWA KUWAUNGA CHADEMA MKONO SAKATA LA KATIBA, SOMA HAPA ALICHOSEMA
Siku chache baada ya Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia kuungana na Chadema pamoja na CUF kupinga kusainiwa kwa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuendesha maandamano nchi nzima, Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye amekiita kitendo hicho kuwa cha kinafiki.
Nape alisema kitendo cha mbunge huyo kuungana na vyama vingine kupinga suala hilo ni kumdhalilisha Rais Jakaya Kikwete aliyemteua kuwa mbunge kwa kumwamini kuwa mchapakazi, huku akiongeza kuwa kitendo hicho ni unafiki mkubwa.
Nape aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM.
Alisema Mbatia aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa mbunge kutokana na kuonekana kuwa mchapakazi, huku akiongeza kuwa kitendo alichokionyesha mbunge huyo ni kumgeuka Rais kama kinyonga
Nape alienda mbali zaidi na kuongeza kuwa hatua ya mbunge huyo kuungana na wapinzani siyo sahihi na haikubaliki hata kidogo, huku akimtaka kujiuzulu nafasi aliyopewa kwa heshima na Rais,.
Katibu huyo mwenezi aliongeza kuwa viongozi wa Chadema wakiwemo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, Dk Willbrod Slaa pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,Tundu Lisu, wamekuwa wakitumia matatizo ya Watanzania kama mtaji wao wa kisiasa na kwamba viongozi hao hawana aibu.
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
WAZALEN
Copyright © 2013 BongoClan™
No comments:
Post a Comment