Obabiyi Aishah Ajibola (kushoto) akivikwa taji hilo mara baada ya kutangazwa mshindi nchini Indonesia.
Mwanamke wa Nigeria amevishwa taji la Mrembo wa Kiislamu Duniani katika fainali ya shindano hilo la urembo lililoandaliwa na kundi la wanawake kupinga mwenendo wa Miss World kwenye shindano lililofanyika nchini Indonesia.
Miss Nigeria, Obabiyi Aishah Ajibola, miaka 21, alishinda shindano hilo la Miss Muslimah World ambalo liliandaliwa na World Muslimah Foundation, kundi la wanawake wa Kiislamu, na kufanyika katika mji mkuu wa Indonesia wa Jakarta katika kupinga utamaduni wa shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwezi huu nchini Bali.
Tukio hilo la kila mwaka la Kiislamu - sasa likiwa katika mwaka wake wa tatu - linafanyika mahsusi kwa wanawake wa Kiislamu, ambao huchunguzwa sio tu mwonekano wao (katika vazi la Kiislamu) lakini pia uchaji Mungu, ufahamu wa dini na uelewa wa Kuran Tukufu.
Zaidi ya wanawake wa Kiislamu 500 waliingia kwenye shindano hilo katika mtandao, huku 20 wakichaguliwa na majaji kuingia fainali. Washiriki walitakiwa kuzungumza na watu kupitia nafasi zao katika dini na ushungi kichwani unamaanisha nini kwao.
Pale Mrembo wa Nigeria alipotangazwa kuwa mshindi - na kushinda safari ya kwenda Makka - alikariri aya kutoka kwenye Kuran Tukufu.
Wakati huohuo huko Bali, mwelekeo wa shindano hilo ulikumbana na upinzani kutoka kwa Waislamu wenye msimamo mkali ndani ya nchi hiyo maarufu zaidi kwa Uislamu, japo waandaaji walitulia na kukubali kufuta kipengele cha vazi la ufukweni.
Licha ya hayo, fainali yake - itakayofanyika Septemba 28 - ilipangwa kufanyika mjini Jakarta, lakini sasa imekubalika kwamba shindano lote litafayika nchini Bali, kisiwa chenye wakazi wengi wa Kihindu, ambako polisi wenye silaha wametapakaa kila kona kufuatia vitisho kwamba shindano hilo litakuwa kitovu cha mashambulio ya ugaidi.
1 comment:
duhhh noma sana
Post a Comment